Uvinza FM

Majangili wawili wakamatwa

12 October 2021, 5:57 pm

Na,Glory Paschal

Polisi mkoani Kigoma wamesema kwa nyakati tofauti wamefanikiwa kuwakamata watu wawili wakituhumiwa kujihusisha na ujangili Pamoja na uhalifu mwingine katika matukio mawii tofauti yaliyotokea Oktoba tisa katika Wilaya za Kibondo na Uvinza

Kamanda wa Polisi Mkoa wa KigomaJAMES MANYAMA, amesema katika tukio la kwanza huko katika Kijiji cha Mkolonga na Kata ya Itebula Tarafa ya Nguruka wilayani Uvinza,askari polisi wakiwa doria ya kuzuia uhalifu walimakamata mwanaume mmoja mkazi wa Uvinza anayejihusisha na matukio ya ujangili

Sauti ya kamanda wa polisi Kigoma

Katika tukio lingine Kamanda MANYAMA amesema huko katika Kijiji cha Busunzu Tarafa ya Kifura wilayani Kibondo, polisi wamemkamata mtuhumiwa wa uhalifu akiwa na pembe ya Ndovu yenye uzito wa kilo moja na nusu ambayo thamani yake haijajulikana akiwa ameificha nyumbani kwake kitendo ambacho ni kinyume cha sheria

Sauti ya kamanda wa polisi Kigoma

Hilo ni tukio la pili kuripotiwa kwa siku za hivi karibuni likihusisha ujangili ambapo Kamanda Manyama amesema polisi kwa kushirikiana na hifadhi za Taifa TANAPA, wataendeleza mapambano dhidi ya ujangili.