Serikali mbioni kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana
07/10/2021, 5:53 pm
Na,Glory Paschal
Waziri wa Nishati JANUARY MAKAMBA amesema serikali iko katika mchakato wa kuhakikisha inafikisha umeme wauhakika Mkoani Kigoma kwa kuunganisha Mkoa huu na Gridi ya Taifa kutoka vituo vya Nyakanazi na Tabora
Mh. MAKAMBA amesema hayo wakati alipotembelea Kituo cha Kuzalisha umeme cha Bangwe na Kasulu ili kujionea hali ya uzalishaji wa umeme kwa mkoa wa kigoma kufutia tatizo la umeme kukatika mara kwa mara Mkoani hapa
Naye Mkurugenzi wa Tanesco Nchini MAHARAGE CHANDE hatua zimeshaanza kuchukuliwa kwa kupunguza baadhi ya njia za umeme zilizokuwa zinategemea umeme na kuwa wameongeza uzalishaji wa mega wat 8.75 ili kuongezza nguvu ya upatikanaji wa umeme
Katika hatua nyingine akiwa wilayani Kasulu Waziri Makamba amesema serikali imetoa shilingi bilioni moja kati ya bilioni sita zinazohitajika ili kuongeza upatikanaji wa umeme katika mji wa kasulu ambao mitaa 76 haina umeme kwa sasa.