Wajasiriamali wametakiwa kutunza mazingira
29 September 2021, 7:29 pm
Na,Glory Paschal
Wajasiriamali nchini wametakiwa kuzingatia elimu ya utunzaji wa mazingira inayotolewa na baraza la uhifadhi wa mazingira NEMC ili kuweka mazingira safi na salama.
Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi mkuu wa NEMC Nchini Bw. Samwel Gwamaka wakati akiongea na waandishi wa habariĀ wakati wa maonesho ya sido kitaifa yanayoendelea wilayani kasulu mkoani kigoma
Bw. Gwamaka ameeleza kuwa katika maonyeosho hayo wanatarajia kukutana na wajasiliamali mbalimbali na kuwapatia elimu ya utunzaji wa mazingira ili kuyalinda hasa wakati wakitekeleza majukumu yao
.
Kwa upande wake Meneja wa nemc kanda ya magharibi Bw. Benjamin Dotto amesema malengo ya nemc ni kuhakikisha kukuaji wa viwanda vidogo unazingatia utunzaji wa mazingira yaliyo Rafiki kwa viumbe hao