Majambazi watatu wauawa
29 September 2021, 6:34 pm
Na,Glory Paschal
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limefanikiwa kuwaua watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi katika barabara inayotokea kijiji cha Kagerankanda kata ya Nyakitonto Tarafa ya Buhoro wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Jeshi la polisi Kasmishina msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma ACP JAMES MANYAMA amesema tukio hilo limetokea September 28 mwaka huu.
Aidha Kamanda MANYAMA ameongeza kuwa miongoni mwa majambazi ho watatu wametoroka huku Jeshi hilo limefanikiwa kukamata Bunduki aina ya AK 47 pamoja na mapanga mawili yaliyokuwa yakitumiwa na majambazi hao.
Katika Hatua nyingine kamanda MANYAMA amesema juhudi za kuwasaka majambazi hao watatu waliotoroka zinaendelea huku akiwaomba wananchi kutoa ushirikiano.
Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa uhifadhi, Hifadhi ya Gombe YUSTIN NJAMASI amesema kuwa jukumu lao ni kuzuia matukio kabla hayajatekelezwa na komba ushirikiano baina yao na wananchi uendelezwe.