Serikali kuja na mpango harakishi wa kila mwananchi kupata chanjo
27 September 2021, 6:48 pm
Na, Mwanaid Suleiman
Serikali imesema imekuja na mpango harakishi wa kuhamasisha chanjo ya corona ikiwa lengo ni kuhamasisha kila mwananchi anapatiwa chanjo ya corona
Hayo yamesemwa na DR CRESENCIA JOHN kutoka ofisi ya mganga mkuu mkoani kigoma wakati akizungumza na kipindi cha amka na redio uvinza fm ambapo amesema mpango huo uanweza kuwafata wananchi nyumba kwa nyumba
Kwa upande wake DR. HOSEA WILIAM amesema kuwa wamejipanga vyema kuelimisha wananchi kwa wale ambao hawana uelewa juu ya chanjo ya corona
kwa mkoa wa kigoma chanjo ilizinduliwa tarehe 3 mwezi 8 huku uitikiaji wa uchomaji chanjo ukiwa bado ni hafifu , ikiwa hadi sasa watu waliojitokeza kuchoma chanjo kwa mkoa wa huu ni watu 5913 na kwa wilaya uvinza ikiwa ni 651.