Wafungwa na watumishi wa gereza wapokea chanjo ya uviko 19
8 September 2021, 5:43 pm
Na,Glory Paschal
Wafungwa na watumishi katika gereza la bangwe mjini kigoma, wamepokea chanjo ya uviko 19 kwa kuchwanjwa ili kuendelea kujilinda na maambukizi ya ugonjwa huo na kuendelea kujilinda na kuwalinda ndugu jamaa na marafiki wanaowatembelea gerezani
Wamesema hatua hiyo ni baada ya kamati ya tafiti na machapisho ya kisanyansi TANFREA kutoa elimu kwa wafungwa na uongozi wa gereza hilo, ambapo wameamua kuchanja chanjo ya uviko 19 kwa hiari ili kujikinga na maambukizi kama anavyoeleza SAULI MAYANGE ambaye ni mkuu wa gereza msaidizi gereza la Bangwe
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya tafiti na machapisho ya kisayansi TANFREA Dkt SAUMU NUNGU amesema licha ya kamati hiyo kuhusika na ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa ya mlipuko na matukio yenye athari za kiafya katika jamii wameanza kuelimisha jamii kuona umuhimu wa kuchanjwa chanjo ya uviko 19 ili kujilinda na maambukizi
Aidha Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Daktari SAIMON CHACHA ameeleza mpango uliopo kuwa, ni kuzifikia taasisi za umma na kutoa huduma ya Chanjo kwa hiali ikiwemo wakimbizi katika kambi za wakimbizi kwa kuwa pia, wanaingiliana na Raia wengine ili kuhakikisha wanakuwa salama.