Uharibifu wa miundombinu ya maji mkongoro bado unaendelea
7 September 2021, 8:17 pm
Na,Glory Paschal
Licha ya Kuundwa Jumuiya za watumia maji katika baadhi ya kata Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwa lengo la kutoa taarifa ya uharibifu wa miundombinu ya maji katika mradi wa Maji wa Mkongoro Namba mbili bado uharibifu unaendelea.
Hayo yambainishwa na Meneja wa wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA, Mhandisi RESPISIUS MWOMBEKI , ambapo amesema baadhi ya watu wasio waminifu wamekuwa wakiharibu Miundombinu hiyo hali inayorudisha nyuma maendeleo.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. BONIPHAS CHUZURA , ameyataja Maeneo ambayo bado yanaongoza kwa uharibifu huo Ikiwemo Kata ya Simbo hali inayosababisha ukosefu wa maji kuendelea kuwepo.
Naye Mratibu wa Mradi wa Maji wa Mkongoro namba mbili Bw. ABEL LUTEMBA mesema ili kuondoa hali hiyo kuna kila sababu ya kuweka ulinzi shirikishi itakayojumuisha kundi la Jumuiya hizo za watumia maji na wananchi.