Uvinza FM

Dawa ya kupunguza makali ya Vvu yaanza kutolewa

3 September 2021, 5:57 pm

Na,Glory Paschal

Dawa ya kupunguza Makali ya  virusi vya UKIMWI imeanza kutolewa kwa miezi sita kwa wagonjwa wenye maambukizi ili kusaidia kupunguza makali ya virusi hivyo.

Hayo yamezungumzwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Saimon Chacha, nakusema wagonjwa waliowengi wamekuwa na uelewa wa matumizi sahihi ya dawa hizo hivyo wameona ni vyema wapewe kwa miezi sita.

Sauti ya mganga mkuu Kigoma

Mratibu wa Shughuli za Ukimwi Mkoani Kigoma Dkt. Hosea William, amesema Mpango wa tatu wa dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi utasaidia watu ambao wamekuwa hawazingatii matumizi bora ya dawa.

Sauti ya mratibu wa vvu kigoma

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu milioni 37 wanaishi na virusi vya VVU, ambavyo husababisha UKIMWI na  zaidi ya robo tatu wako Nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.