Shirika la afya WHO latoa msaada wa baiskeli 100
19 August 2021, 4:34 pm
Na,Glory Paschal
Shirika la afya Duniani, WHO limetoa msaada wa baiskeli 100 Mkoani Kigoma kwaajili ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii waliopo katika maeneo ya mipakani na katika kambi za wakimbizi ili kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa ya mlipuko
Akikabidhi baiskeli hizo kwa Mganga mkuu wa mkoa Kigoma zenye thamani ya shilingi millioni 27.7 Mratibu wa WHO Kigoma, Dkt Jailos Hiriza amesema baiskeli hizo zitakwenda katika wilaya zote nane ili kuendeleza mapambano dhidi ya magonjwa ya Mlipuko
Amesema wamelenga kupeleka baiskeli hizo katika maeneo hayo kutokana na urahisi wa kupenyeza magonjwa ya mlipuko na kusambaa katika jamii
Sekta ya afya mkoani hapa inakiri kuwa uwepo wa baiskeli hizo utasaidia wahudumu wa afya ngazi ya jamii kufika maeneo ya mbali ambayo yalikuwa ni changamoto katika kufikisha elimu ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Covid 19