Wafanyabiashara wa vyombo vya moto waiomba serikali kushusha bei ya mafuta
13 August 2021, 7:31 pm
Na,Rosemary Bundala
Wafanyabiashara wa vyombo vya moto vya usafiri kutika kijiji cha Ruchugi wilayani uvinza mkoani kigoma wameiomba serikali kuwa tatulia suala la kupanda kwa bei ya mafuta kutokana na hali ya kiuchumi ilivyo kwasasa.
Wakizungumza na redio uvinza fm wafanya biashara hao wamesema kuwa hali kwa sasa sio nzuri kiuchumi hivyo wanaiomba serikali iweze kupunguza bei hiyo ili iwasaidie kupata pesa ya ya kujikimu na maisha ambapo mafuta hayo kwasasa yamepanda kutoka 2,400 hadi kufikia 2,700.
Nae Raphael Mgaya ambae ni katibu mtendaji wa Tanzania Association of oil Marketing Companies (Taomac) amaelezea sababu zilizopelekea mafuta hayo ya petrol kupanda bei.
Kupanda kwa mafuta ya petrol ni agizo lililotolewa na Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) ambapo ilitangaza bei kikomo za bidhaa ya mafuta ya petrol hapa nchini ambapo zilianza julai 1 mwaka huu ikiwa ni kuendana na sheria ya fedha ya mwaka 2021.