Waliopokea chanjo ya uviko 19 afya zao ni salama
11 August 2021, 7:29 pm
Na,Timotheo Leornadi
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ruchugi kata ya Uvinza wilayani Uvinza Mkoani Kigoma ambao tayari wamepokea chanjo ya UVIKO -19 wamesema ni salama kwa afya, nakwamba wale ambao bado wanamitazamo hasi wakachajwe kulinda maisha yao
Hayo wameyasema kwa nyakati tofauti ndani ya kijiji hicho wakati Redio Uvinza fm ilipotaka kujua maendeleo ya wananchi ambao tayari wamepokea chanjo na wale ambao hawajapokea chanjo hiyo
Kwa upande wake mganga Mkuu wa Wilaya ya Uvinza BI: ZAITUNI HAMZA amesema hadi sasa hawajapokea malalamiko yoyote kuhusu chanjo hiyo huku akisisitiza wananchi kuendelea kuchanja
Hata hivyo Daktari Hamza ameendelea kusema kuwa takwimu kwa maeneo ambayo wamefika kutoa chanjo ndani ya wilaya ya uvinza zimeongezeka tangu walipoanza zoezi hilo
Aidha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MH. SAMIA SULUH HASAN hivi karibuni alizindua chanjo ya corona kwa kuchanjwa yeye kwanza ilikuwathibitishia watanzania kuwa hakuna madhara kwa watakaoitumia.