Serikali kutenga fedha kwa ajili ya kutengeneza barabara
28/05/2021, 7:15 pm
Na,Rosemary Bundala
Serikali imesema itaendelea kutenga fedha katikaWizara ya ujenzi ili kuzifanyia matengenezo barabara korofi kwa kadri upatikanaji wa fedha utakavyokuwa unaendelea kuimarika
Hayo yamejili leo bungeni jijini Dodoma wakati naibu waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) Mh David Silinde alipokuwa akijibu swali la mbunge wa kigoma kusini mh Nashon William Bidyanguze lililohoji je serikali ina mpango gani wa kujenga barabara tatu za lukoma lubalisi, kaliya, lubanda na kaliasibwe zinazounganisha mkoa wa kigoma kupitia wilaya ya uvinza
Aidha katika hatua nyingine mh Silinde amesema katika mwaka wa fedha 2019/2020 barabara za lukoma , lubalisi,kalia lubanda na kalia sibwesa zilitambuliwa na wakala wa barabara za vijijini na mijini TARURA na kuwekwa kwenye mfumo unaotambuliwa na TARURA na barabara hizo zitaingizwa kwenye mpango wa matengenezo ya barabara kupitia fedha za matengenezo ya barabara zinazotolewa na TARURA katika kila halmashauri
Katika hatua nyingine naibu waziri amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na wananchi pamoja na shirika la maendeleo la ubeligiji la kuendeleza kilimo kigoma linaendelea na ujenzi wa madaraja kumi kwa kutumia tekinolojia ya mawe kwa gharama ya shilingi milioni 190 ambapo madaraja matatu yamekamilika likiwemo daraja la mto luega katika barabara ya kalia lubanda lililojengwa kwa shilingi milioni thelathini na saba katika mwaka wa fedha 2019/2020