Serikali yaahidi kuwalinda raia na mali zao
27 May 2021, 5:32 pm
Na,Rosemary Bundala
Serikali imesema inaendelea kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika na kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku kwa amani na utulivu
Hayo yamejiri leo bungeni jijini Dodoma wakati waziri mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la mbunge wa makete mh Festo Richard Sanga lililohoji je ni ipi kauli na maelekezo ya serikali dhidi ya vitendo vya uhalifu vinavyoendelea katika taifa letu
kwa upande mwingine mh waziri kassim majaliwa amesema anavipongeza vyombo vyote vya dola nchini kwa kuendelea kufanya kazi kwa juhudi katika kuhakiksha usalama wa wananchi na mali zao unaendelea
Katika hatua nyingine waziri mkuu amesema ni jukumu la kila mtanzania kuhakikisha kuwa anashiriki kikamilifu kwenye ulinzi wa nchi pale anapoona kuna dalili za upotevu wa amani ni vyema kutoa taarifa kwenye vyombo vya ulinzi
Bunge limeeendelea leo jijini Dodoma ambapo wizara mbalimbali zimekwisha wasilisha bajeti zake .