Wananchi waiomba Serikali kudhibiti maeneo hatarishi
27 May 2021, 4:55 pm
Na,Glory Paschal
Wananchi Mkoani Kigoma wameitaka Serikali kudhibiti maeneo hatarishi ya mito na mabwawa machafu yanayochochea ongezeko la magonjwa ya kichocho na minyoo hasa kwa watoto
Wamesema maeneo mengi yamejaa maji Machafu hivyo ni muhimu elimu ikatolewa kwa kuwashirikisha wananchi na serikali za mitaa na vijiji ili kuokoa maisha ya watu ambayo yapo hatarini kutokana na hali hiyo
Mratibu wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele Mkoani Kigoma Emmanuel Bihongora amesema katika kukabiliana na magonjwa ya minyoo na kichocho watatoa dawa kwa watoto kuanzia umri wa miaka mitano kuhakikisha wanadhibiti magonjwa hayo
Kwa upande wake mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina ameitaka jamii kutumia fursa hiyo kuhakikisha watoto wote wanapata dawa ili kudhibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele