Uvinza FM

Wananchi walia na zahanati

17/05/2021, 5:30 pm

Na,Timotheo Leonardi

Wananchi wa Kitongoji cha Kazaroho Kijiji cha Ruchugi Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma wameiomba serikali kuwajengea Zahanati katika kitongoji hicho, ilikuondoa usumbufu ambao wamekuwa wakikutananao kinamama wajawazito, kwa kutembea umbali mrefu hali ambayo hupelekea wakati mwingine kujifungulia njiani

Zahanati

Wakizungumza na Redio Uvinzafm mara baada ya kuwatembelea Wananchi hao wamesema  wanalazimika kutembea umbali wa kilomita zaidi ya sita usiku na mchana kufuata huduma ya afya

Sauti za wananchi

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Wilaya ya Uvinza Dkt. ZAITUN HAMZA amesema kuwa kinamama wajawazito wanaotembea umbali mrefu hupelekea  kutopata huduma kwa wakati nakwamba nidhamira ya serikali kuhakikisha inasogeza huduma karibu na wananchi ili kupunguza vifoo vitokanavyo na ujauzito

Sauti ya Mganga mkuu Uvinza

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Ruchugi amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ya kutembea kwa umbali mrefu nakueleza jitihada wanazozifanya kuhakikisha wanawajengea Zahanati Wananchi hao.

Sauti ya Mwenyekiti