Jumuiya ya Dini yatoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu
28/04/2021, 6:18 pm
Na,Glory Paschal
Jumuiya ya Dini Mbalimbali Mkoani kigoma imetoa Pongezi kwa Mh. Rais Samia Suluhu kwa kuwa Rais wa Tanzania na kuvipa nafasi vyama vya siasa vya Upinzani kupata fursa ya kuonana nae na kuzungumzia mwenendo wa Siasa Nchini
Jumuiya hiyo inahusisha dini ya Kiislamu na kikristo pamoja na madhehebu ya pande zote mbili lengo likiwa ni kuendelea kudumisha amani, umoja na Upendo katika kulijenga Taifa
Kisha pongezi kwa Mh rais Samia Suluhu Hassan kwanza kwa hotuba yake aliyotoa bungeni iliyoonyesha dira ya Tanzania ambayo kila mwananchi anatamani kuifikia lakin kubwa Zaidi ni mustakabali wa siasa nchini kwa kutoa nafasi ya kukutana na viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye na Mkuu wa Wilaya Uvinza wakapongeza jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa na viongizo wa dini na kuwaomba kuendeleza juhudi za pamoja kuhakikisha malengo ya serikali yanatimia.