Uvinza FM

Zaidi ya Wanafunzi 600 wafundishwa na Walimu 8

23 April 2021, 4:51 pm

Na,Timotheo Leonardi

Shule ya Sekondari Ruchugi iliyopo Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa walimu hali inayopelekea wanafunzi kupata wakati mgumu kufanya vizuri kwenye mitihani yao

Shule ya Sekondari Ruchugi

Hayo yamebainishwa na mkuu wa shule ya Sekondari Ruchugi Godwin Omela wakati Akizungumza na Redio Uvinzafm ambapo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo huku akisema walimu hao waliopo hawajitoshelezi kwani shule hiyo inauhitaji wa walimu 26 ili kuweza kukidhi mahitaji ya wanafunzi waliopo

Mkuu wa Shule ya Ruchugi

Kwa upande wao wanafunzi wamesema wanapata wakati mgumu wakujifunza kutokanana uhaba huo uliopo hasa katika masomo ya sayansi licha ya hivyo wanazidi kupambana ili kupata ufaulu mzuri katika mitihani yao

Wanafunzi wa Shule ya Ruchugi

Hata hivyo aprili 9 mwaka huu kupitia kwa naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi David Silinde Wakati akijibu swali la msingi la Mbunge Bungeni Jijini Dodoma alisema wamepanga kuajiri walimu 6000  kujaza mahali ambapo kuna uhaba.