Shilingi 7.3bilioni kutengeneza mtandao wa barabara
23 April 2021, 4:15 pm
UVINZA
Na,Editha Edward
Wananchi katika wilaya ya UVINZA mkoani Kigoma wameiomba serikali kupitia TARURA kuongeza kasi katika ujenzi wa barabara ya Uvinza mjini ili Kuruhusu shughuli za kiuchumi za wananchi kufanyika kwa urahisi
Wakizungumza na Radio Uvinza Baadhi yao wamesema Pamoja na jitihada zilizopo za TARURA kujenga miundombinu ya barabara Bado kuna maeneo yasiyopitika kutokana na ukosefu wa madaraja katika Baadhi ya Mito jambo linaloathiri shughuli zao zikiwemo za Biashara Kufayika
Mratibu wa TARURA mkoa wa Kigoma Mhandisi Godwin Mpinzile amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021 kiasi cha shilingi bilioni 7.3 kimeidhinishwa kwa ajili ya ujenzi wa mtandao wa barabara na madaraja kwa mkoa wa Kigoma huku milioni 400 kwa mwaka 2021 zikiwa zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa madaraja wilaya ya Kigoma ambapo hadi sasa madaraja 15 yamekamilika na ifikapo Juni mwaka huu madaraja 20 yanatarajiwa kuwa yamekamilika