Kilio cha Walemavu chatatuliwa
16 April 2021, 3:35 pm
UVINZA
Na, Editha Edward
Baada ya Redio uvinza fm kuripoti taarifa ya watu wenye ulemavu kupatiwa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na kila halmashauri kwa takribani miezi mitano iliyopita ili kujikwamua kiuchumi halmashauri ya wilaya ya uvinza mkoa wa kigoma imetoa mkopo kwa makundi maalumu wanawake,vijana na watu wenye ulemavu zaidi ya milioni Themanini
Akizungumza katika hafla ya utoaji mikopo hiyo iliyofanyika jana katika ukumbi wa biashara uliopo wilayani hapa mkuu wa mkoa wa Kigoma kamishina wa polisi THOBIAS ADENGENYE ambaye ndo alikuwa mgeni rasmi amesema mikopo hiyo iliyotolewa kwa makundi hayo itawasaidia na kuwabadilisha maisha yao endapo pesa hizo watazifanyia shughuli za kimaendeleo
Naye mkuu wa wilaya ya Uvinza Bi.MWANAMVUA HOZA MRINDOKO amesema vijana na watu wenye ulemavu wamekuwa hawajitokezi kwa wingi katika fursa hiyo ya kuchukua mikopo hivyo amewataka kujitokeza ili waweze kunufaika
Kwa upande wao wanufaika wa mikopo hiyo ambao miongoni mwao ni watu wenye ulemavu wamesema wanaishukuru serikali kwa kuwathamini licha ya kuwachukua muda mrefu wa kupata mikopo hiyo tangu walipoiomba
Aidha halmashauri ya Wilaya uvinza imefanikiwa kutoa mikopo kwa makundi maalumu ikiwa ni asilimia mia moja tangu sheria ya fedha ilipofanyiwa marekebisho.