Wananchi wa Kibirizi wawashukuru Viongozi wao
16 April 2021, 1:27 pm
Na; Glory Kusaga
KIGOMA
Wananchi wa kata ya Kibirizi Manispaa ya kigoma ujiji wamewashukuru Viongozi wa kata hiyo kwa jitihada za kudhibiti matukio ya wizi na udokozi yaliyokuwa yanaathiri Maendeleo yao .
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema Vitendo vya wizi vimekuwa kikwazo cha maendeleo yao kwa mda mrefu na kwamba jitihada za viongozi kushughulikia wahalifu imekuwa msaada mkubwa kuimarisha ulinzi na usalama wao.
Aidha Wameomba vyombo vya Usalama kuendelea kuwashirikisha wananchi katika Kuwabaini waharifu na kuwatolea Taarifa ili waweze kuchukuliwa Hatua na kuimarisha Ulinzi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na Taifa.
Kwa upande wake afsa mtendaji wa kata ya Kibirizi Bw. Richard Sarehe Magayi amepongeza namna wananchi wanavyotoa ushirkiano kwa viongozi na kwamba wataendelea kuwashirikisha wananchi ili kumaliza kabisa Vitendo vya wizi na udokozi katika kata ya Kibirizi.