RUWASA Manyara yawataka wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji
3 January 2025, 5:37 pm
Meneja Ruwasa mkoa wa Manyara James Kionaumela amesema serikali imeweka mkakati wa kila jimbo kupewa visima vitano ambapo kwa mkoa wa Manyara kuna visima 35 na mpaka sasa vimeshachimbwa visima 29 na wanaendelea na uchimbaji wa visima vilivyobaki.
Na Mzidalfa Zaid
Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(RUWASA) mkoa wa manyara imesema kwa kipindi cha mwaka 2025 imejipanga kusambaza huduma ya maji kwenye vijiji ambavyo havina maji.
Meneja Ruwasa mkoa wa Manyara James Kionaumela amesema serikali imeweka mkakati wa kila jimbo kupewa visima vitano ambapo kwa mkoa wa Manyara kuna visima 35 na mpaka sasa vimeshachimbwa visima 29 na wanaendelea na uchimbaji wa visima vilivyobaki
Kionaumela amewataka wananchi kulipia bili za maji ili mamlaka ijiendeshe yenyewe kwa kuwalipa mafundi ambao wanafanya ukarabati pindi inapotokea changamoto ya miundombinu kuharibiwa.
Aidha, amewataka wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji, kwa kutofanya shughuli za kiuchumi karibu na vyazo hivyo ikiwemo kukata miti, kuchunga mifugo au kulima.