Mbunge wa Bububu atembelea vikundi vya wakulima Mbuzini
13 December 2024, 6:46 pm
Na Mwandishi Wetu.
Mbunge wa Jimbo la Bububu, Mwantakaje Haji Juma, amefanya matembezi, kuangalia hatua za maendeleo na kutathimini changamoto kwa wakulima wa mboga mboga wa Mbuzini na Dole wilaya ya Magharibi A Unguja.
Akiwa katika shamba la kikundi cha Wema hauozi cha Mbuzini amesema kuwa anafurahishwa na wakazi hao kwa uamuzi wao wa kujumuika pamoja na Kuazisha harakati za kilimo ambacho ndio mkombozi maisha kwa watu.
Mbunge amewashauri viongozi wa kikundi hicho kufikiria kuazisha jumuiya au asasi ya kiraia itakayofanya shughuli za kilimo na uhifadhi wa mazingira ili kuwa na uwanja mpana wa kufanya harakati za kilimo, kutoa elimu pamoja na kufanya shughuli za uhifadhi wa mazingira na kuoambana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mwenyekiti wa kikundi cha Wema hauozi Suleiman Khamis Haji amesema kuwa changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa ni kuwa na eneo dogo la kufanyia harakati zao, na wamemuomba Mbuge huyo kuwafikiria namna ya kuitatua changamoto hiyo.
Naye katibu wa kikundi hicho Mkali Juma Makame amesema kuwa, wamepikea wazo na wameahidi kulifanyia kazi haraka iwezeoanavyo ili kunanua shughuli zao kwa upana zaidi katika ngazi ya wilaya na nchi kwa ujumla.
Amesema kuwa kwa sasa kikundi cha Wema hauozi kina wanachama 25, wanawake 17 na wanaume wanane (8) ambao wanalima mboga mboga, kutengeneza udogo wa kuwatikia, kutengeneza mbelea ya mboji na bokashi.
Ameongeza kuwa kikundi cha Wemahauozi kimesajiliwa katika wilaya Magharibi A na kuruhusiwa kufanya shughuli za kilimo na hadi sasa kimepatiwa mafuzo ya ukulima na taasisi mbali mbali kama vile ZARI, PPIZ na Idara ya Kilimo ya Zanzibar.
Kwa sasa wakulima hao wanalima pilipili, mchicha, mnavu, nyanya chungu, mapapai, nanaa, mint na mboga nyengine za aina mbali mbali katika eneo la Mbuzini.
Mbunge huyo ametembelea vikundi vya wakulima mboga mboga Dole, kikundi cha wakulima mboga mboga Mbuzini kwa Sepetu na wakulima kikundi cha Wema hauozi Mbuzini.