JUMAZA yatoa zaka Kusini Unguja
11 December 2024, 3:53 pm
Ni kawaida ya Jumaiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) kukusanya zaka kutoka kwa waumini wa dini ya Kiislam na kuwapatia wahitaji mbalimbali Zanzibar.
Na Ali Khamis
Bodi ya ZAKA na SADAKA ya Jumuiya ya Maimanu Zanzibar (JUMAZA) imetoa zaka ya mali kwa kuwapa mitaji ya shughuli ndogo za kiuchumi wahitaji waliofanyiwa tathmini na jumuiya hiyo, katika Shehiya za Muyuni, Wilaya ya Kusini, Mkoa Kusini Unguja.
Mjumbe wa bodi ya zaka JUMAZA, Yassin Ameir amesema kuwa watu wenye mahitaji ni wengi hivyo ni lazima kwa watu wenye uwezo wa fedha na mali, kutoa ZAKA kwani ni miongoni mwa nguzo kuu ya uisloamu, hivyo ni wajibu kwa waisilamu kuitekeleza ili kupunguza umasikini katika jamii.
Katibu wa bodi ya zaka JUMAZA, Nassor Miraj Shaib amesema kuwa, jumla ya wanufaika wanne wamekabidhiwa vitendea kazi na fedha taslimu kutokana na mapendekezo yaliyotolewa na kila mmoja kutokana na mradi anaokusudia kufanya. Sheha wa shehiya ya Muyuni B, Rashid Abrahaman Rashid amesema kuwa ameishukuru jumuiya ya maimamu Zanzibar kwa kuchagua eneo la Shehiya za Muyuni kutoa Zaka hiyo na kusema kuwa wanufaika waliopewa mitaji, wafanye shughuli walizopendekeza ili kuingiza kipato kama ilivyokusudiwa.