Adhana FM
Adhana FM
20 October 2025, 12:19 pm
Na Juma Haji wa Adhana FM Wasilamu wenye nia ya kwenda kuhijji Makka, Saudi Arabia mwaka 1448 hijiria wametakiwa kujiandaa kusoma elimu ya hijja kabla ya ili kupunguza changamoto zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa ibada hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Masjidi Jamiu Zinjibari Mazizini mjini Unguja kadhi wa mahakama ya rufaa Zanzibar fadhilatu shekh Iddi Saidi Khamis, amesema kutokana na upekee wa Ibada ya hija kutekelezwa mara moja kwa mwaka upo umuhimu kwa waislam kujiunga na madarasa yanayosomesha elimu ya ibada iyo ili kuwa na uhakika wa kufuzu ibada hiyo.
Amesema hujajji mwenye kutekeleza nguzo zote za hija kwa ukamilifu wake, hupandishwa daraja na Mwenyezi Mungu, ya kuzibali ibada zake pamoja na kumulipa pepo siku ya hesabu.
Amesema wapo baadhi ya waislam kwa kuto kusoma ibada ya hija mapema hulazimika kufanya ibada kwa kuiga na hivyo kukosa kuwa wanyenyekevu kwa mola wao.
Akifungua kikao hicho Mkurugenzi wa wakfu, Amana na Hijja kutoka wakfu na mali ya amana Zanzibar Hajjat Madina Haji Khamis amezitaka taasisi zinazosafirisha mahijajji chini ya taasisi ya UTAHIZA kuongeza kasi ya kutoaji wa elimu ya hijja kwa mahujaji kwa kuwa taasisi hizi ndizo zenye dhamana ya kuhakikisha kila hujaji anahiji kwa uhakika na kupata malipo ya ibada hiyo kwa Alah.
Nae Dr Naufal Kasim Mohamed, mkuu wa kamati ya Afya kwa mahujaji ameseka ili hija ikamilike nin vyema taasisi za kusafirisha mahujaji kufanyakazi ya kupima afya za mahujaji mara kwa mara ili kutoa mahujaji wenye uwezo wa kutekeleza vyema ibada hiyoMaandalizi ya ibada ya hija ya mwaka huu yanaendelea hatua kwa hatua hapa Zanzibar na November 4 mwaka 2025 yataendelea kwa mambo ya nje ya Tanzania ambapo Serekali ya itafunga mkataba na Serekali ya Saudi Aradia ili kuruhusu shughuli za mahujaji kuendelea Nchini saudia Arabia
