Adhana FM
Adhana FM
29 June 2025, 8:39 pm

Na Khamis Ali
Wahariri na wasimamizi wa tovuti ya taasisi ya habari za maendeleo TADIO kutoka kanda ya Zanzibar wameshauriwa kuwazingatia watu wenye ulemeavu ili kuondoa dhana potofu kwa jamii.
Akitoa mada ya vyombo vya habari na watu wenye ulemavu, mkufunzi Tuma Dandi kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania TBC amesema kuwa katika jamii ipo mitazamo hasi na unyanyapaa dhidi wa watu wenye ulemavu hivyo ni muhimu kwa vyombo vya habari kuuelimisha umma kuhusu fikra potofu juu ya ulemavu kwani kila kundi katika jamii linayo tafsiri yake kuhusu ulemavu.
Amesema kuwa, waandishi wa habari wanapokwenda kuwahoji watu wenye ulemavu kwa ajili ya kupata taarifa, waulize maswali ambayo hayawanyanyapai ili wawe huru kueleza maoni yao yatakayoifaidisha jamii na kusaidia kuondoakana na fikra mbaya dhidi ya makundi ya watu wenye ulemavu.
Said Omar said kutoka redio Jmaii Mkoani amesema kuwa katika vipindi vyao vya redio wameweka utaratibu wa kuaandaa haabri zinazohusu watu wenye ulemavu ili kutoa fursa kwa makundi hao kushiriki katika kutoa maoni yao kwa jamii.
Naye Amua Rushita, Mkufunzi na msimamizi wa tovuti ya vyombo vya habari vya kijamii Tanzania TADIO amesema kuwa TADIO kwa kushirikiana na VIKES wameona ni vyema waandishi kuandika habari za watu wenye ulemavu zinazohusu maendeleo kwani katika kundi hilo, wapo watu wenye vipaji mbali mbali vyenye faida kwa jamii.
Mafunzo hayo, yameingia katika mzunguuko wa tatu tokea kuasisiwa kwake mwaka 2021 katika kuwanoa na kuwakumbusha watendaji wa tovuti hiyo inayotumika kuchapisha na kutiririsha matangazo kwa vituo vya redio vipatavyo 47 vya kijamii vya Tanzania bara na Zanzibar ambapo hadi sasa yametolewa kwa waandishi wa vituo vya redio kutoka kanda za Dar es Salaam, Mbeya, Dodoma, Mwanza na Zanzibar.