Adhana FM
Adhana FM
28 June 2025, 1:11 pm

Na Nishan Khamis
Waandishi wa habari nchini wametakiwa kutumia kalamu kutetea haki za wanawake wanaojitokeza kugombea nafasi za uongozi, kwa kuripoti na kukemea vitendo vya vurugu na udhalilishaji, kuelekea uchaguzi mkuu.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania – Zanzibar (TAMWA ZNZ), Dk. Mzuri Issa, wakati wa mafunzo maalum ya siku moja yaliyofanyika hapo jana katika ofisi za chama hicho huko Tunguu, yakihusisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari visiwani Zanzibar.
Dk. Mzuri amesema waandishi wana nafasi ya kipekee ya kuhakikisha wanawake wanaingia katika ulingo wa siasa na uongozi bila hofu ya kukumbana na unyanyasaji wa aina yoyote.
Aidha, mesisitiza kuwa licha ya uwepo sheria na sera nzuri za kwalinda wanawake bado wanahabari wanalo jukumu la kipekee la kuwalinda wanawake dhidi ya vitendo viovu katika uchaguzi ili kuondoa mazingira ya hofu kwa jamii ya wanawake nchini.
