Adhana FM
Adhana FM
18 April 2025, 5:10 pm
Na Juma Haji – Zanzibar
Afisi ya Raisi, Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar inakusudia Kufanya Uzinduzi na Utekelezaji wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa kisheri ya Mama Samia katika Mikoa Mitatu ya Zanzibar iliyobakia kufikiwa na Kampeni hiyo ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kufikisha huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi wote.
Akizungumza na redio Adhana FM kwenye kipindi maalum cha kuitambulisha Kampeni ya msaada wa kisheria kwa wananchi Afisa sheria kutoka Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria katka Ofisi ya Rais katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora bora Zanzibar Bw Hamid Hamadi Juma ameitaja mikoa itakayofkiwa na Kampeni hiyo ni pamoja na Mkoa wa kaskazini Unguja, Mkoa wa kusini Unguja na Mkoa wa Kusini Pemba.
Amesema kwa Mkoa wa kaskazini Unguja Kampeni itazinduliwa tarehe 23 April 2025, Mkoa wa kusini Unguja tarehe 3 May 2025 na kwa Mkoa wa kusini Pemba ni tarehe 5 May 2025.
Aidha Amesema idara imejipanga kufikisha Wataalam mbali mbali kwenye mikoa hiyo katika siku za kampeni watakao kuwa na uwezo wa kukabiliana vyema na utatuzi wa matatizo yatakayowasilishwa na wananchi.
Kampeni hii ya msaada wa kisheria itahusisha Utoaji wa elimu, usikilizaji na utatuzi wa maswala mbali mbali ya kisheria ikiwemo elimu ya kujikina na ukatili wa kijinsia migogoro ya ardhi, migogoro ya ndoa na talaka, upatikanaji wa vyeti za kuzaliwa na vitambulisho vya ukaazi ambapo kauli mbiu ya Kampeni hiyo ni msaada wa kisheria kwa Haki, Usawa, Amani na Maendeleo.
Kampeni ya msaada wa kisheria Nchini Tanzania inaendeshwa na Wizara ya Katiba ya jamuhuri ya muungao wa Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais katiba, Sheria, Utumishi na utawala bora Zanzibar.