Adhana FM
Adhana FM
3 April 2025, 5:28 pm

Na Juma Haji Adhana FM
Umoja wa Taasisi za Hijja Zanzibar (UTAHIZA) umetangaza kuwa ifikapo18 April 2025 kuwa mwisho wa kupokea maombi ya VISA kwa waumini wanaotaka kwenda kutekeleza Ibada ya hija ya mwaka 1446 hijria.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari huko katika ukumbi wa Masjid Nur-Muhamad uliopo kwa mchina mwazo, Wilaya ya magharibi “B” Unguja mwenyekiti wa kamati ya hijja ya UTAHIZA, Shekh Ali Adam Ali amesema hatua hiyo imekuja kufuatia makubaliano yaliyopo kati ya taasisi hiyo na taasisi zinazosimamia hijja huko Makka Saudi Arabia ili kurahisisha kuratibu shughuli za usafirishaji wa mahujaji.
Amesema lengo la taarifa hii ni kuwataarisha watu wenye nia ya kushiriki ibada hiyo mwaka 2025 kukamilisha taratibu zilizopangwa ikiwemo kufanya malipo kwa wakati.
Amesema mtu yoyote ataewasilisha maombi yake nje ya muda uliopongwa hatopata nafasi ya kushiriki ibada ya hijja na atapangiwa kushiriki ibada hiyo hapo mwakani.
Aidha Aalim huyo amewaomba wale wote wenye nia ya kushiriki ibada hiyo kuendelea kukamilisha taratibu hizo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.
Jumla ya mahujaji 3380 kutoka Tanzania wanatarajiwa kushiriki ibada ya hijja ambapo kwa Zanzibar ni mahujaji 2460 na kwa upande wa Tanzania- bara ni 920,