Adhana FM
Adhana FM
1 April 2025, 7:03 am

Na Mwandishi Wetu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Iddi.
Sala Hiyo imefanyika Msikiti wa Jamiu Zenjibar Kiembe Samaki Wilaya ya Magharibi B.
Akizungumza katika Hutuba ya Sala ya Iddi Imam wa Msikiti huo Sheikh Khamis Gharib Khamis amewasisitiza Waislamu kumdhihirisha Mwenyezi Mungu kwa Kutenda Mambo mema yenye Kuleta furaha, Mapenzi na Umoja Miongoni mwao.
Amefahamisha kuwa inawapasa Waislamu Kuendeleza Tabia Njema pamoja na Kumcha Mungu kwani kuna Manufaa Makubwa Mbele ya Mwenyezi Mungu .
Imam Khamis amewanasihi Waumini wa Dini ya Kiislamu kutovuka mipaka katika Kusherehekea Sikukuu ya Idd na Kuepuka mambo maovu.
Aidha Alhaj Dkt,Mwinyi amekutana na Masheikh mbalimbali kutoka Mikoa yote Unguja na Pemba waliofika Ikulu kusalimiana naye na kutakiana Heri ya Sikukuu ya Iddi.
Alhaj Dkt, Mwinyi amewashukuru Masheikh hao kwa Kazi Mzuri walioifanya wakati wa Mwezi wa Ramadhani kwa Ibada na Mafundisho mbalimbali pamoja na Sala ya Tarawehe na kusisitiza Ushirikiano na Utaratibu huo kuendelezwa.
Alhaji Dkt, Mwinyi amewaomba Viongozi hao wa Dini ya Kiislamu Kuendelea kuiombea Dua Nchi pamoja na Viongozi Wakuu Ili ibaki na Amani wakati wote.
Wakati huohuo Alhaj Dkt,Mwinyi ametoa Mkono wa Iddi kwa Wananchi mbalimbali ikiwemo Watoto Waliofika Viwanja vya Ikulu.
Amewatakia kila la Kheri wakati huu wa Kusherehekea Sikukuu ya Idd el Fitr.