Halmashauri ya CCM Kaskazini Unguja yaridhishwa na utekelezaji miradi ya maendeleo
5 July 2024, 5:37 pm
Na Juma Haji Adhana FM
Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja imesema imeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi inayoendelea kufanywa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Mmkoa huo.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Ndugu Iddi Ali Ame katika ziara maalumu ya wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM ya mkoa huo yenye lengo la kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ndani ya Mkoa huo.
Amesema halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Kaskazini Unguja imeridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo hasa kwa kuwa imelenga kutatua changamoto za wananchi.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Rashid Hadidi Rashid amekishukuru Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kuitembelea miradi hiyo ili kuona namna ambavyo serikali inavyosimamia utekekezaji wa ilani ya CCM kwa kwa wananchi.
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wa mkoa huo wameishukuru Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kazi nzuri inayoifanya kwenye utekelezaji wake wa ilani ya chama chao.Jumla ya miradi saba imetembelewa ikiwemo Mradi wa Hoteli ya Nyota Tano Pwani Mchangani, Soko la Mkwajuni Mradi wa Tangi la Maji Bumbwini, Bohari ya Gesi(Oryx),Mangapwani ,Bohari ya Mafuta Mangapwanii, uandaaji wa vitalu vya ujenzi wa misingi na uchimbaji wa visima kibokwa pamoja na Skuli ya Ghorofa .