Adhana FM

Mahujaji waliosafiri na Jumuiya ya Istiqama, wawasili Muzdalifa

15 June 2024, 10:35 pm

Na Mwandishi Wetu

Kiongozi wa Kamati ya Hijja ya Jumuiya ya Istiqama, Sultan Khamis Al Mazroui amewaongoza mahujaji waliosafiri na kundi lao kuondoka viwanja vya Arafa na kuwasili Muzdalifa baada ya kukamilisha nguzo kuu ya Hijja.

Sheikh Sultan amesema kuwa, wameondoka Arafa baada ya kuzama kwa jua ambapo watalala Muzdalfa kwa ajili ya kujiandaa na ibada nyengine.

Naye Sheikh Farid Salum Abdallah amesema kuwa mahujaji wote waliosafiri na Istiqama wamewasili Muzdalifa wakiwa na afya njema na wamefika huko katika makurdi ya awali.

Mahujaji hao watakaa Muzdalfa usiku kucha kesho asubuhi wataelekea Jamarat kwa ajili ya kutupa vijiwe.