Adhana FM

Mwili ya mwanamme wakutwa ukielea bwawa la Bandamaji

4 June 2024, 7:34 pm

Na Abdul Sakaza, Wilaya ya Kaskazini “A”

Kijana anayefahamika kwa jina la Nada Faki Khamis (38) mkazi wa Kinyasini wilaya ya Kaskazini “A” mkoa Kaskazini Unguja umekutwa ukielea katika bwawa la Bandamaji baada ya kufariki dunia.

Akithibitisha tukio hilo, kamanda wa Kikosi cha Zima Moto na Uokozi (KZU) mkoa Kaskazini Unguja Kamanda Asha Othman amesema, mnamo majira ya saa saba na nusu za mchana, walipokea taarifa ya kuonekana mwili ukielea katika bwawa eneo la Banda maji na kufanya juhudi za kuuopoa kwenye maji mwili huo wa marehemu majira ya saa nane za mchana ukiwa tayari umeshaaza kuharibika na mwili na kuupeleka katika hospital ya wilaya ya Kivunge kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Nae Mkuu wa wilaya Kaskazini “A” Othman Ali Maulid alifika katika eneo hilo na amewataka wananchi kua makini wakati wanapofanya shuhuli zao katika mito na mabwawa mbali mbali ili kujiepusha na madhara ya matukio ya aina hiyo.

(Imeandikwa na Abdul Sakaza na kuhaririwa na Ali, Khamis M )