Waratibu wa shehiya watakiwa kushikamana kutatua changamoto za wanawake-Waziri Pembe
2 June 2024, 4:09 pm
Na Juma Haji, Adhana FM
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto Zanzibar Riziki Pembe Juma, amesema waratibu wa shehia wana nafasi kubwa ya kushikamana katika kutatua changamoto za wanawake na watoto ili kuwaepusha na janga la ukatili na udhalilishaji.
Kauli hiyo ametoa huko katika ukumbi wa kwa wazee seblen Amani wilaya ya mjini, wakati akifunguwa kikao cha waratibu wa jinsia katika Shehia za Unguja.
Ameshauri waratibu hao, kujikita zaidi kutoa elimu katika jamii na sio kusubiri mpaka matokeo ya udhalilishaji kuathir jamii kwa kushindwa kufuatiliwa mapema.
Kwa uapnde wake Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya jamii, jinsia na watoto Siti Abasi Ali amesema, idara yake imeweka utaratibu wa kukutana kila baada ya miezi 4 ili kujadili masuala mbalimbali ya wanawake na Watoto.
Amesema vikao hivyo, ni chachu ya kuwaunganisha pamoja waratibu hao na ni fursa pekee kwao katika kupanga mikakati ya kutoa elimu ya udhalilishaji kwenye jamii.
Nao Waratibu hao, wameiomba Serikali kuwatatulia changamoto ya utelekezaji wa Wanawake na Watoto, kuwepo kwa makundi ya vijana wahuni pamoja na ukosefu wa vitambulisho maalum vya kufanyia kazi ili kuepuka matatizo yanayowakabil baadhi yao ikiwemo mashirikiano madogo kutoka kwa Masheha na Jeshi la Polisi
(Imeandikwa na Juma Haji Juma na kuhaririwa na Ali, Khamis M)