Wanahabari wahimizwa kuongeza elimu kwa ufanisi wa kazi zao
31 May 2024, 8:51 am
Na Nishan Khamis, Wilaya ya Mjini.
Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharib Idrisa kitwana Mustafa amewahimiza waandishi wa habari Zanzibar kuongeza elimu ili kuendana na mabadiliko ya siku hadi siku.
Kitwana amesema hayo katika shughuli ya utoaji wa tunzo kwa waandishi wa habari vijana iliyofanyika Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar – SUZA katika skuli ya cha habari kilimani.
Ameeleza kuwa mfumo unaotumiwa SUZA wa kuwashindanisha vijana kuandika habari kwa kuzingatia ubora wa uhariri utasaidia kuimarisha umahiri katika tasnia ya habari.
Mkuu wa mkoa amesema kuwa tasnia ya habari ni muhimili wa nne wa nchi kutokaa na umuhimu wake hivyo lazima wandishi wazingatie sheria pamoja na maadili ili kuepuka kuingia katika matatizo.
Mkuu wa idara wa idara ya mawasiliano na mafunzo ya habari -SUZA, Dkt Khamis Juma amesema kuwatunuku tunzo waandishi wa habari vijana (18 -35) ikiwa ni tunzo za kwanza kutolewa SUZA kutatoa hamasa kwa vijana na kuleta tija katika jamii.
Dkt Khamisi alieleza kuwa Malaka za runinga, redio, magazeti na vipeperushi zitasaidia kuleta umahiri katika kazi na kuleta mageuzi makubwa vijana kwenye sekta mbali mbali ikiwemo, uchumi wa buluu, elimu, afya na Mazingira kwa ujumla.
Aidha ameeleza kuwa walioshiriki katika tunzo hizo jumla yao ni 40 kati ya hao washiriki 17 kazi zao zimeingia katika ushindani wa kuwania tunzo ambapo wanawake ni 10 wanaume ni saba.
Kwaupande wake Kaimu Balozi mdogo wa China nchini Tanzania amesema ushirikiano wa china na Zanzibar unazidi kuimarika katika masuala ya elimu, afya, utalii pamoja na utamaduni.
Hivyo amesema hali hii itasaidia kuongezeka kwa fursa za masono kwa wanafunzi wanaotoka Zanzibar (Tanzania) kwenda China kujifunza mambo mbalimbali na kubadilishana uzoefu wa lugha ya kiswahili na kichina kwa vitendo.
Nao washiriki na washindi katika katika tukio hilo wamesema hatua hiyo siyo mwisho bali wataendelea kutumia kalamu zao kwa maadili na ubunifu zaidi katika kuisadia jamiii kwa misingi ya maendeleo nchini.
(Imeandikwa na Nishan Khamis na kuhaririwa na Ali, Khamis Mtwana )