Makamo wa pili wa Rais: Mpango wa Pensheni jamii umewasiadia kiuchumi baadhi ya wazee walio wengi nchini.
2 October 2021, 8:46 am
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla ameitaka jamii kuweka kipaumbele jukumu la kuwalea wazee na kuwapa matunzo na huduma za msingi.
Hemed ametoa kauli hiyo katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wazee duniani kilichofanyika katika Uwanja wa Skuli ya Kitope Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema wazee wanahitaji mapenzi na huruma kutoka kwa Watoto na jamii inayowazunguka hivyo ni lazima kwa familia na jamii kuhakikisha wazee wanaishi katika hali ya furaha, amani na mapenzi.
Alieleza kuwa, kuwalea wazee ndani ya nyumba ni jambo linaloleta baraka na fanaka sambamba na kutoa mafunzo mema kwa Watoto.“Tufahamu kwamba vitabu vitakatifu vinaeleza umuhimu na baraka ya kuwatunza wazee, Na tufahamu kuwa ukimtendea maovu mzee wako Mwenyezi Mungu anakuja kukulipa maovu na wewe” Alieleza Mhe. Hemed
Makamu wa Pili wa Rais aliesema katika kuunga mkono suala hilo Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais Dk. Mwinyi imeendelza dhamira na shabaha ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuweka mikakati ya kuwaendeleza wazee ambayo inaendelea kuimarishwa na kwa kuendelea kuwatunza wazee wasiokuwa na jamaa wala rasilimali katika makazi maalum ikiwemo Sebleni, Welezo na Limbani.
Alieleza, Mpango wa Penchini jamii umeweza kuwasiadia kiuchumi baadhi ya wazee walio wengi kwa kuzitumia fedha hizo katika shughuli ndogo ndogo za uzalishaji mali na kujiongezea kipato.
Alisema wazee waliopo katika vituo hivyo Serikali inaendelea kuwapatia huduma zote za msingi wanazostahiki ikiwemo kuwasimamia, chakula, malazi ,mavazi matibabu pamoja na posho.
Alieleza kwamba, Idara yenye dhamana na wazee imehakikisha inaendelea kuwasajili wazee wote waliofikia umri wa miaka sabiini na wananufaika na pensheni hiyo,ili iendelee kuwasaidia katika shughuli zao za kila siku.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kuimarisha huduma za wazee ikiwemo afya na usafiri , na kueleza kuwa kwa hatua ya awali jumla ya wazee Elfu mbili mia nne na arubaini na nane (2,448) wameshapatiwa vitambulisho maalum vya kuwasaidia kupata huduma hizo kwa urahisi.
Akisoma risala kwa niaba ya wazee Maulid Nafasi Juma alisema wazee wa Zanzibar wanampongeza Rais Dk. Mwinyi kwa kuendeleza Jitihaza zilizoanzishwa na Serikali ya awamu na sab ana kuahidi kuendelea kumuunga mkono Mhe. Rais katika kupambana na vitendo viovu ikiwemo kupiga vita suala la ubadhilifu wa mali za umma.
Alisema Pamoja na mipangoz mizuri ya serikali lakini bado wazee wanakabiliwa na baaadhi ya changamoto ikiwemo wazee kubebeshwa tuhuma za uchawi ndani ya jamii, uchakavu wa majengo wanayoishi wazee, Pamoja na kuanywa nyuma katika utekelezaji wa baadhi ya mipango ya kisekta.
Aidha, katika risala hiyo, wazee waliishauri serikali kushusha umri wa wazee katika kuopkea pencheni jamii ili iweze kutoa fursa kwa wazee wengi Zaidi waweze kupata penchini hiyo Pamoja na kuanzishwa kwa dirisha maalum katika vituo vya Afya kwa ajili ya kuwahudumia wazee.
Nae, Mkurugenzi wa Shirika la kuwahudumia wazee Duniani nchini Tanzania (Help Age International) Smart Daniel Alipongeza serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuanzisha program maalum ya pencheni jaamii jambo ambo limepelekea baadhi ya nchi katika bara la Afrika kuiga jambo hilo ikiwemo nchi ya Kenya na Uganda kwa upande Nchi za Afrika Mashariki.
Alieleza, kauli mbiu ya mwaka huu inalenga kuwashirikisha wazee katika kuchangia pato la taifa hasa katika matumizi ya kidigitali.Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Matumizi Ssahihi Ya kidijitali Kwa Ustawi wa rika zote”.