Uvinza FM

Mbinu zinazochangia upotevu wa mazao shambani

3 February 2026, 2:06 am

Mazao yanayopotea baada ya kuvuna. Picha na Ai

Kila msimu wa mavuno unapofika, mashamba mengi vijijini hujaa tabasamu na matumaini ya maisha bora, lakini nyuma ya furaha hiyo kuna ukweli usioonekana kirahisi. Jasho la mkulima la miezi mingi mara nyingi huishia kupotea shambani, si kwa sababu ya ukame au mafuriko, bali kutokana na mbinu hafifu za uvunaji wa mazao. Mahindi na maharage mazao tegemeo kwa chakula na kipato huanza kuharibika mara tu yanapovunwa kwa njia zisizo sahihi, na hivyo kupunguza thamani ya kazi yote iliyofanyika msimu mzima.
Karibu usikilize makala hii maalum inayokufungua macho kuhusu namna mbinu duni za uvunaji zinavyopelekea upotevu mkubwa wa mazao mashambani.