Uvinza FM

Wakulima Uvinza waomba fedha za kimataifa ziwafikie

19 November 2025, 12:57 am

wakulima wakiwa wanaelekezwa kilimo cha kuhifadhi mazingira

Na. Abdunuru Shafii

Karibu kusikiliza Makala fupi inayozungumzia kwa kina athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi katika kilimo nchini Tanzania, hususan katika Wilaya ya Uvinza na Mkoa wa Kigoma. Wakulima wamekuwa wakikumbana na mabadiliko yasiyotabirika ya mvua ikiwemo vipindi virefu vya ukame na vipindi vya mvua kubwa zinazoleta uharibifu hali ambayo imeathiri kwa kiasi kikubwa mavuno na kusababisha uhaba wa chakula pamoja na kupungua kwa uzalishaji wa kibiashara.

Na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na watetezi wa mazingira inaendelea kutafuta ufadhili, ikiwemo ruzuku zinazoweza kufikia dola milioni 20 kwa kila mradi kutoka taasisi za kimataifa kwaajili ya Mfuko wa Fidia kwa Hasara na Uharibifu (Loss and Damage Fund) kupitia mazungumzo ya COP ili kukabiliana na changamoto hizi za tabianchi.