Uvinza FM
Uvinza FM
7 October 2025, 4:14 pm

“Wazee wa Uvinza wengi hawana bima za msamaha hivyo kupata changamoto ya matibabu wanapopata maradhi nipe ridhaa ya kuwa diwani”
Na Dunia Stephano
Mgombea udiwani kata ya Uvinza kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM Nillis Ntabaye amesema endapo atapewa ridhaa ya kuongoza kata iyo atahakikisha anaweka kipaumbele kwenye upatikanaji wabima za afya za wazee ili waweze kupata matibabu kwa wakati.
Amesema hayo alipokuwa akinadi sera zake kwenye mkutano wa kampeni na wananchi wa kata hiyo ambapo amesema kuwa wazee wa Uvinza wengi hawana bima za msamaha hivyo kupata changamoto ya matibabu wanapopata maradhi.
Sauti mgombea Udiwani BIMA Wazee
Aidha amesema atasaidia kuleta pampu itakayovuta maji ilikusaidia upatikanaji wa maji katika kata ya Uvinza pia kwa maeneo kama karwera, irunde na tandala kutachimbwa visima vya sola na umeme.
Sauti mgombea udiwani Maji
Kwa upande wake Mgombea udiwani viti maalumu tarafa ya nguruka Bi. Pili Musa Kapomorola amesema atapambania wanawake na vijana kupata mikopo ya asilimia kumi.

Sauti Mgombea viti maalumu
katika hatua nyingine katibu wa umoja wa vijana UVCCM Saidi kaki amewataka wananchi kupiga kura kwa Amani na bila kushiriki kwenye migogoro ya aina yoyote.
Pamoja na hayo kampeni za uchaguzi zinaendelea huku viongozi mbalimbali wakiendelea kunadi sera zao kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 mwenzi wa kumi mwaka huu.