Uvinza FM
Uvinza FM
29 September 2025, 11:42 pm

“Nina uwezo wa kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wananchi wa kata ya uvinza nipeni ridhaa ya kuwa diwani wenu tukafanye kazi kwa maslahi ya Wanauvinza”

Na Theresia Damasi
Mgombea udiwani wa Kata ya Uvinza kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Himidi Kisobwe, amewataka wanachi wa kata ya uvinza kumpa ridhaa ya kumchagua kuwa diwani wa kata hiyo ili kufanikisha sera na vipaumbele vyake ikiwemo, elimu,maji na ajira kwa vijana.
Bw. Kisobwe ameyasema hayo wakati akizungumza na uvinza fm redio katika kipindi cha kumekucha ambapo ameahidi kushirikiana na wananchi ili kuhakikisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi ikiwa ni pamoja na kutatua migogoro ya ardhi .
Sauti ya mgombea Bw. Kisobwe
Ambapo Miongoni mwa ahadi ambazo ametaja kukamilika kwa barabara ya Karuele hadi Shekeshe kuwa ni kipaumbele chake kikuu na kusema barabara hiyo ni kiungo muhimu kwa shughuli za kiuchumi na kijamii, hivyo kukamilika kwake kutarahisisha usafirishaji wa mazao na huduma nyingine.
Aidha, Kisobwe ameweka wazi kuwa atafanya tafiti na kushughulikia changamoto za majia ambazo zimewakabili wananchi kwa mda mrefu bila utatuzi ambapo uvinza imezungukwa na vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na mto ruchugi na malagarasi.
Sauti ya mgombea Bw. Kisobwe
Kwa upande wa mwenyekiti wa chama hicho kata ya uvinza Bw Erasto Bidya Shabani amesema chama kimempa ridhaa mgombea udiwani kupitia chama chao kwa kuwa na maono na mipango endelevu ya kuipaisha kata ya uvinza bila kujali itikadi ya vyama.

Sauti ya mwenyekiti wa chama Act Wazalendo kata ya uvinza Bw Erasto Bidya Shabani
Ikumbukwe kuwa kampeni za uchaguzi zinaendelea nchini kwa wagombea kunadi sera za ilani za vyama vyao ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika oktoba 29,2025.