Uvinza FM

Mwenge wa Uhuru 2025 Kugusa Miradi ya Bilioni 2.4 Uvinza

22 September 2025, 2:01 pm

Mkuu wa wilaya ya Uvinza Dinnah Mathamani akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu wa wilaya ya kigoma Rashidi Chuachua

‎Mwenge wa Uhuru utakimbizwa ndani ya wilaya kwa umbali wa kilomita 131

Na Abdunuru Shafii

Jumla ya miradi 7 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2.4 inayojumuisha sekta za elimu, afya, Maji na nishati inatarajiwa kukaguliwa, kutembelewa na mingine kuwekewa jiwe la msingi katika mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 katika Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma. ‎‎

Akizungumza wakati wa kusoma taarifa ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza,  Bi. Dinnah mathamani, amesema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa ndani ya wilaya kwa umbali wa kilomita 131, kuanzia katika viwanja vya Shule ya Msingi Mapinduzi kijiji Cha Mlela hadi katika viwanja vya  shule ya msingi Kachiringulo, Kijiji Cha Uvinza.‎‎

Bi. Dinnah mathamani amesema kuwa ata hakikisha  wa Mwenge wa Uhuru katika kuhamasisha maendeleo, mshikamano na amani miongoni mwa wananchi, pamoja na kuwa chombo muhimu cha kuhamasisha ushiriki wa jamii katika shughuli za kijamii na kiuchumi.‎

Ikumbukwe Mwenge wa Uhuru mwaka huu umebeba kaulimbiu yenye ujumbe thabiti “Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu.”‎