Uvinza FM
Uvinza FM
15 August 2025, 6:57 pm

Waziri wa madini Athony Mavunde pamoja na watumishi wengine wa serikali wakikagua chumvi inayodhalishwa katika kiwanda cha nyanza salt uvinza
Waziri mavunde amesema Kiwanda cha Nyanza kina msaada mkubwa katika kuchangia pato la taifa na kuzindua chumvi lishe ya wanyama ni mwanzo mzuri wa maendeleo nchini.
Na Theresia Damasi
Waziri wa madini Anthony Mavunde amezindua bidhaa mpya ya chumvi lishe ya mifugo {cattle Lick} katika kiwanda cha chumvi nyanza salt katika wilaya ya uvinza mkoani Kigoma ambapo bidhaa hiyo itakuwa inasaidia mifugo kuwa na afya nzuri na virutubisho,ambapo hapo awali wafanyabiashara nchini Tanzania walikuwa wanaagiza kutoka nje ya nchi.

Akizindua bidhaa hiyo Waziri mavunde amesema Kiwanda cha Nyanza kina msaada mkubwa katika kuchangia pato la taifa na kuzindua chumvi lishe ya mifugo ni mwanzo mzuri wa maendeleo nchini na kwa mkoa mzima wa kigoma.
Sauti ya Waziri wa madini Athony Mavunde
Waziri Mavunde amesema amefarijika kuzindua bidhaa ya cattle Lick ya mifugo hivyo anawaomba wafanyabiashara kuwaunga mkono nyanza salt kwa kazi kubwa ambayo wanayoifanya na kuacha kuagiza bidhaa hiyo nje ya nchi kwani tayari bidhaa inapatikana nchini.
Sauti ya Waziri wa madini Athony Mavunde
Kwa upande wake Dinnah Mathamani Mkuu wa wilaya ya uvinza amesema kiwanda cha nyanza salt kina mchango mkubwa wa kupandisha uchumi katika wilaya ya uvinza kwani kimezalisha ajira kwa asilimia kubwa na kwa upande wa masoko kinaongeza ufanisi wa ndani na nje.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya uvinza Dinnah Mathaman
Kadhalika mkurugenzi mkuu wa halmashauri ya uvinza Fred Milanzi amesema bidhaa ya cattle lick katika halmashauri yake ni fursa kwani wafugaji ni wengi huku ufugaji ukiendelea kukua ambapo anamatumaini bidhaa hiyo inaenda kuwa mkombozi kwa wafugaji wote ambapo mifugo inaenda kuwa na afya.
Sauti ya Mkurugenzi wa halmashauri ya uvinza Fredi Milanzi
Nao baadhi ya wananchi na wafanyakazi waajiriwa katika kiwanda cha Nyanza salt wameeleza manufaa wanayoyapata hasa kujipatia riziki kwa njia ya ajira waliyonayo katika kiwanda hicho ambapo kupitia fursa hiyo familia zinapata mahitaji yote na kujikwamua kiuchumi.

Picha ni wafanyakazi na wadau wakiwa katika uzinduzi wa bidhaa mpya ya lishe ya mifugo katika kiwanda cha chumvi
Hata hivyo kiwanda cha Nyanza salt kipo wilaya uvinza katika mkoa wa kigoma kimetoa ajira kwa wazawa wa mkoa wa kigoma na ambao sio wazawa kwa asilimia kubwa pia kinachangia pato la taifa kwa ukubwa wenye maendeleo endelevu.