Uvinza FM
Uvinza FM
27 June 2025, 4:53 pm

Afisa Afya na Mazingira Hussein Kateranya akiwa katika studio za uvinzafm redio akitoa elimu juu ya kufanya usafi wa mazingira.Picha na Ezra Meshack.
“Utaratibu wa kufanya usafi ni jukumu la kila mtu katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama ili kujilinda dhidi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu”.
Na Theresia Damasi
Serikali ya halmashauri ya wilaya uvinza imewataka wananchi wa halmashauri hiyo kuzingatia kanuni na taratibu za kufanya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ili kuepukana na adhabu zitakazotolewa ikiwa ni pamoja na kupigwa faini.
Utaratibu wa kufanya usafi ni jukumu la kila mtu katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama ili kujilinda dhidi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu pamoja na ugonjwa wa malaria.
Akizungumza na Uvinza fm Redio ,Afisa Afya na Mazingira wa halmashauri ya wilaya ya uvinza Bw. Hussein Kateranya amesema jamii inapaswa kufahamu umuhimu wa kufanya usafi mara kwa mara katika mazingira wanayoishi,Sehemu za biashara, Masoko na Maeneo ya vyanzo vya maji.
Sauti ya Afisa Kataranya 1
Kateranya ameeleza kwa kina athari zinazoweza kutokea endapo jamii haitazingatia usafi na utunzaji wa mazingira ambapo amesema kunaweza kutokea kwa mabadiliko mabaya ya hali hewa ambayo yataleta athari kwa wananchi.
Sauti ya Afisa Kataranya 2
Aidha Kateranya amesema jamii inapaswa kufahamu mazingira ni nini na kufuata taratibu zilizowekwa na serikali katika kutunza mazingira na kufanya usafi katika maeneo yao na sehemu za biashara.
Hata hivyo Afisa Kateranya amesema serikali haitakuwa na huruma kwa mtu yeyote atakayekiuka utaratibu wa kufanya usafi katika maeneo yake, ambapo amesema kila mmoja azingatie wajibu wake kama mwananchi.
Sauti ya Kateranya 3