Uvinza FM
Uvinza FM
26 June 2025, 4:02 pm

Diwani wa kata ya Uvinza katika Halmashauri ya wilaya ya uvinza Bi. Aloca Mashaka ametoa ripoti ya utekelezaji wa miradi mbalimbali aliyoifanya katika kata yake mara baada ya miaka mitano ya uongozi wake.

Na Theresia Damasi
Diwani wa kata ya Uvinza katika Halmashauri ya wilaya ya uvinza Bi.Aloca Mashaka ametoa ripoti ya utekelezaji wa miradi mbalimbali aliyoifanya katika kata yake toka alipochaguwa na wananchi kwa miaka 5 ya uongozi wake.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo ya barabara ya kasulu katika kijiji cha uvinza,Bi. Aloca Mashaka amesema lengo la mkutano huo ni kuwaaga wananchi mara baada ya kuvunjwa kwa baraza la madiwani tarehe 20 june 2025.
Bi. Aloka Mashaka amesema kuwa katika kipindi cha kipindi cha miaka mitano amefanikiwa kusimamia ujenzi wa shule ya uvinza sekondari kwa asilimia 99.4 ambapo amesema hiyo imetokana na pesa za shule zilizokuwa zimepangwa katika shule ya sekondari Ruchugi.
Sauti ya Mh. Diwani Aloca Mashaka
Aidha Bi.Aloca amejibu maswali yaliyoulizwa na mwananchi anayefahamika kwa jina la Wikey John wakati wa mkutano huo wa hadhara ikiwemo suala la uwepo wa gari la kubebea wagonjwa katika kata yake.
Sauti ya Mh. Diwani Aloca Mashaka
Kwa upande wake Mtendaji wa kata ya uvinza Edward Amos amesema katika kata yake wamefanikiwa kujenga shule mpya za msingi (6) na shule mpya za sekondari 2.
Sauti ya Afisa Mtendaji
Aidha Bw. Edward Amos amewataka vijana wa kata ya uvinza kuchangamkia fursa za ajira na kuacha kulalamika mtaani.

Ikumbukwe kwamba baraza la madiwani halmashauri ya wilaya uvinza limevunjwa tarehe 20 june 2025 kwa lengo la kuhitimisha na kutoa ripoti ya ilani ya chama tawala na miradi mbalimbali iliyotekelezwa.