Uvinza FM

Wananchi watakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya m-pox

25 March 2025, 9:10 am

Diwani wa wa Kata ya Kumunyika na viongozi mbalimbali wakiwa katika mkutano wa hadhara katika kata ya Kumunyika. Picha na Emmanuel Kamangu

Diwani wa wa kata ya kumunyika Bw. Seleman Kwirusha kutoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanajikinga na ugonjwa hatari wa homa ya nyami kwa kufuata taratibu za kiafya.

Na. Emmanuel Kamangu

Diwani wa wa kata ya kumunyika ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa kasulu Bw, Seleman Kwirusha amewataka wananchi wa kata hiyo kuchukua tahadhari zidi ya ugongwa wa homa ya nyani M pox.

Diwani kwirusha ametoa wito huo  wakati wa mkutano wa hadhara katika kata ya kumunyika , mkutano ambao umelenga kujadili mambo mbali mbali  ya maendeleo ya kata hiyo ambapo ametumia mwanya huo kutoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanajikinga na ugonjwa hatari wa homa ya nyami kwa kufuata taratibu za kiafya.

Sauti ya Diwani wa wa kata ya kumunyika Bw, Seleman Kwirusha

Kwa upande wake kaimu mganga mkuu halmashauri ya mji wa kasulu Bw, Augustine Karoli akiwa katika mkutano huo amethibitisha kuwepo kwa wagonjwa  wa homa ya nyani katika mji wa kasulu na kuwasihi wananchi kuepuka kusalimiana kwa kugusana, kukumbatiana ,na kujitahidi kuvaa barakoa ili kukabiliana na ugonjwa huo.

Sauti ya kaimu mganga mkuu halmashauri ya mji wa Kasulu Bw, Augustine Karoli

Nao baadhi ya wananchi wa kata ya kumunyika ambao wameshiriki mkutano wa hadhara  wamesema kwa elimu ambayo wamepewa watajitahidi kuchukua tahadhari huku wakiomba waendelee kupewa elimu zaidi  juu ya ugonjwa wa homa ya nyani.

Sauti za wananchi wa kata ya Kumunyika

Dalili za ugonjwa wa homa ya nyani ni pamoja na maumivu ya kichwa , kutokwa na mapele mwili mzima, misuli kukaza, madonda ya koo na kulegea kwa mwili