Uvinza FM

Vijana wapewa Elimu ya utotoleshaji kwa njia ya asili

5 February 2025, 10:06 pm

vijana wa kike na wakiume wakiwa wanapata mafunzo ya ufugaji na utotoleshaji, picha na Abdunuru Shafii

vijana wamefanikiwa kupata Elimu ya ufugaji bora, Elimu ya utotoleshaji kwa kutumia njia za asili (Kinengunengu), Kupanda malisho kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na Elimu ya kuchanja hasa ugonjwa wa kideri.

Mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wa kike na kiume kutoka kata za Mganza, Mtegowanoti, Kazuramimba, Kadanga na Mwakizega  wilayani Uvinza, yalifanyika kwa siku katika ukumbi wa Romani Catholic uliopo kata ya Uvinza katika Halmashauri ya Wilaya ya uvinza.

Mafunzo hayo yalikuwa na lengo la kutoa Elimu na kuwajengea uwezo vijana hao. Katika mafunzo vijana wamefanikiwa kupata Elimu ya ufugaji bora, Elimu ya utotoleshaji kwa kutumia njia za asili (Kinengunengu), Kupanda malisho kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na Elimu ya kuchanja hasa ugonjwa wa kideri.

watalaam wa mifugo wakiwa na washiliki wa mafunzo, picha na Abdunuru Shafii

Mafunzo hayo yalitolewa na watalaam wa mifugo kutoka Wizara ya Mifugo Kanda ya mashariki Tabora VIC pamoja na watalaamu wa mifugo katika Halmashauri ya wilaya ya Uvinza.

Hata hivyo vijana walioshiriki mafunzo hayo wameaswa na wataalam kuyafanyia kazi mafunzo bila kukiuka kwani watafaidika kwa kiasi kikubwa.