Wakimbizi 16 Nyarugusu hufariki kila wiki
28 January 2025, 9:30 pm
Wakazi wengi katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu wana uhaba mkubwa wa vyandarua.
Na Emmanuel Kamangu
Wakimbizi 9 mpaka 16 katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma hufariki kila wiki kutokana na ugonjwa wa malaria.
Akizungumza na Uvinza FM, Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu Bw. Siasa Manjenje amesema wakazi wengi katika kambi hiyo wana uhaba mkubwa wa vyandarua jambo linalopelekea walio wengi kushambuliwa na mbu.
Aidha Bw, Manjenje amesema maambukizi ya malaria katika kambi ya Nyarugusu yanachukua asilimia 40 ya magonjwa yote katika kambi hiyo na asilimia hizo zikitajwa kuongezeka tofauti na awali.
Kwa upande wao baadhi ya wakazi katika kambi ya Nyarugusu mmoja wao akiwa Bw, Manimambo wamesema ugonjwa wa malaria unawapa changamoto kubwa ikiwa ni pamoja na kupoteza wapendwa wao.
Hata hivyo wakazi hao wameyaomba mashirika mbalimbali kuwasaidia vifaa tiba hasa vyandarua ili kukabiliana na janga hilo la malaria.