Uvinza FM

Hali tete kwa wafanyabiashara wa ng’ombe

25 January 2025, 2:38 pm

Baadhi ya mifugo katika mnada wa halmashauri ya wilaya ya Uvinza. Picha na Ally Henry

Hali ya kibiashara kuwa ngumu kutokana na mifugo kukosa malisho.

Na Josephine Asenga

Wafanyabiashara katika mnada wa mifugo uliopo katika Halmashauri ya wilaya ya Uvinza wameeleza namna hali ilivyo katika biashara zao kwa mwaka huu wa 2025.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Uvinza fm wafanyabiashara hao na kueleza kuwa changamoto mojawapo wanayokumbana nayo ni pamoja na hali ya biashara kutokuwa nzuri kwani mifugo hukosa sehemu ya malisho.

Sauti za wafanyabiashara wa mifugo.
Mwenyekiti wa mnada wa halmashauri ya wilaya ya Uvinza Bw. Chimdunya. Picha na Ally Henry

Naye mwenyekiti anayesimamia shughuli za biashara zinazoendelea katika mnada huo Bw. Chimdunya ameeleza hatua ambazo ni za kufuata kwa ambaye anakwenda kununua mfugo kwani zipo changamoto ambazo hujitokeza kwa wanunuzi ikiwa ni pamoja na kutapeliwa.

Sauti ya Mwenyekiti wa mnada Bw. Chimdunya.