Wasiozingatia sheria za usalama barabarani kukiona
15 January 2025, 9:45 pm
Mtu yeyote atakayevunja kanuni na taratibu zilizowekwa hata sita kumchukulia hatua za kisheria.
Na Theresia Damasi
Waendesha vyombo vya moto wakiwemo bodaboda wametakiwa kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabarani kwa kuwa na leseni ili kuepukana na changamoto ya kuleta usumbufu jambo ambalo linazua taharuki Mara kwa Mara.
Hayo yameelezwa na Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa kigoma kamishna msaidizi wa polisi[ACP]Philemon Makungu wakati wa akizungumza na uvinza fm kwa njia ya simu, ambapo amesema leseni ni muhimu huku akiongeza kuwa mtu yeyote atakayevunja kanuni na taratibu zilizowekwa hata sita kumchukulia hatua za kisheria.
ACP Makungu amesema uwepo wa ajali nyingi zinazotokea nikutokana na madereva kutozingatia kanuni na taratibu za barabarani,hivyo ili kutokomeza ajali nilazima kila dereva awe na leseni.
Pamoja na hayo Kamanda wa jeshi la polisi huyo amesema mpaka sasa wanaendelea na operesheni ya kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto ili kudhibiti ajali.