Uvinza FM

Mkuu wa wilaya ya Uvinza awataka wanafunzi wote kuripoti shule

13 January 2025, 11:02 pm

Mkuu wa wilaya ya Uvinza Bi. Dinah Mathaman akifanya mahojiano na uvinza fm radio picha na Linda Dismas

awahimiza wazazi kuwajibika kuwapeleka watoto shule.

Na Theresia Damasi

Mkuu wa wilaya ya Uvinza Dinah Marthani amewataka wazazi kutimiza wajibu wao wa kuwapeleka watoto shule na kuacha mara moja tabia ya kuwatumikisha, jambo ambalo ni kinyume na sheria, ikiwa leo rasmi shule zimefunguliwa.

Ameyaeleza hayo wakati akizungumza na radio uvinza fm,katika kipindi cha kumekucha ambapo amesema kuwa kila mtoto ana haki ya kupata elimu,hivyo wazazi/walezi wasilete mzaha kwani sheria itachukua mkondo wake.

Sauti ya mkuu wa wilaya

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Nyambutwe Jen Ndalichako amesema wanafunzi walioripopti shule kwa siku ya leo ni asilimia 80.

Sauti ya mwalimu mkuu Jen Ndalichako

Nao baadhi ya wazazi kutoka halmashauri ya wilaya ya uvinza wameeleza namna wanavyojishughulisha kujiingizia kipato ili waweze kuwatimizia watoto mahitaji ya shule.

Sauti ya wazazi