Wananchi watakiwa kujitokeza kusikiliza sera za wagombea
19 November 2024, 10:11 pm
Ndugu Kisena Mabuba Msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa wilaya ya kigoma mjini amesema wamejipanga vyema kuelekea uchaguzi serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.
Mkurugenzi na msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa manispaa ya Kigoma ujiji Kisena Mabuba ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kusikiliza sera za wagombea kutoka vyama mbalimbali vya siasa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mabuba ameeleza kuwa tayari amepokea ratiba za kampeni za vyama vyote vya kisiasa kwaajili ya utaratibu maalumu na kuepuka migongano katika sehemu mbalimbali za mikutano hiyo, na kusema kampeni za uchagzuzi wa serikali za mitaa zitaanza tarehe 20-26 mwezi novemba 2024, kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni , na tarehe 27 itakuwa siku ya uchaguzi.